KAMPALA, Uganda
AJALI ya basi la shule imesababisha vifo vya wanafunzi 20, pamoja na mtu mzima mmoja, katika eneo la Kapchorwa, Mashariki mwa Uganda.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa basi hilo lilibeba wanafunzi wa Shule ya King David, ikisadiki kuwa huenda mtu mzima aliyefariki ndiye mmiliki wa Shule hiyo.
Chanzo cha ajali hiyo iliyotokea jana Julai 16, 2026, ni gari kumshinda dereva na hatimaye kuacha njia na kugonga jiwe kubwa kando ya barabara.
Inaelezwa kuwa ajali ilitokea wakati wanafunzi hao wakiwa njiani kurudi baada ya ziara ya masomo katika kivutio cha utalii cha Maporomoko ya Sipi.
Uganda ni moja ya nchi za Afrika zinazoshuhudia ajali nyingi za barabarani kila mwaka, huku sababu zikitajwa kuwa ni mwendo mkali, magari yasiyo na ubora, na ubovu wa barabara.


