30.3 C
New York

‘Usikimbilie kuoa kama huna pesa’

Published:

LAGOS, Nigeria

HUO ni ushauri wa staa wa mtandao wa TikTok nchini Nigeria, Amadou Elizabeth Aminata, maarufu kwa jina la Jarvis.

Jarvis amekuja na ujumbe huo kwa vijana kuelekea harusi yake na staa mwenzake wa mitandaoni, Peller.

Katika ushauri wake, bibiye huyo amewataka vijana kujipanga kwanza kiuchumi, kabla ya kukimbilia maisha ya ndoa. “Kama huna pesa, usioe. Nawaomba mjaribu kufanya hivyo,” amesema.

Aidha, Jarvis ametoa ujumbe mwingine kwa vijana watakaoamua kuoa wakiwa na maisha ya kawaida.

Kwa hao, Jarvis amewataka kufunga ndoa za kitamaduni, ambazo kimsingi zina gharama ndogo, ukilinganisha na zile za mikusanyiko mikubwa.

Mrembo huyo na Peller watafanya sherehe Agosti Mosi, 2026, ukiwa ni mwezi mmoja tangu walipofunga ndoa ya kitamaduni mjini Benin, Jimbo la Edo nchini Nigeria.

Related articles

Recent articles