33.7 C
New York

Japan silaha ya Urusi dhidi ya Ukraine?

Published:

NEW YORK, Marekani

URUSI imekuwa ikiitegemea Japan katika teknolojia na udukuzi wakati huu wa vita vyake na Ukraine, kwa mujibu wa ripoti ya Gazeti la New York Times la Marekani.

Chanzo hicho cha habari kimeeleza kuwa baadhi ya makachero wa Urusi wamekimbilia Japan tangu walipofukuzwa katika mataifa ya Ulaya baada ya nchi yao kuivamia kijeshi Ukraine.

Aidha, Times limeenda mbali zaidi na kudai kuwa kampuni za teknolojia za Japan zimekuwa upande wa Urusi tangu vita hivyo viliponza mwaka 2022.

Kabla ya madai hayo, Serikali ya Ukraine iliwahi kusema Urusi imekuwa ikiishambulia kwa kutumia silaha za kivita zinazotengezwa Japan.

Katika utafiti wake, Ukraine ilieleza kuwa kati ya ‘drone’ (ndege zisizo na rubani) 10 zinazotumiwa na Urusi, tisa zinatoka katika nchi hiyo ya Asia.

Kupitia mahojiano yake na Times, mmoja ya makachero wa Ulaya Magharibi, amesema maofisa wa kijeshi wa Urusi wamekuwa wakienda Japan kwa siri.

Katika mahojiano hayo, licha ya kutokutajwa jina, alisema maofisa hao hujifanya wanadiplomasia au wafanyabiashara, huku lengo likiwa ni kununua teknolojia na silaha.

Related articles

Recent articles