26.6 C
New York

Ufaransa inazuilika kutwaa ubingwa?

Published:

PARIS, Ufaransa

BAADA ya ubingwa wa mwaka 2018, safari hii timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa ipo tena kwenye nafasi ya kutwaa taji hilo katika fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea.

Timu hiyo imeshinda mechi zote sita ikizifunga Senegal, Iraq, Norway, Sweden, Paraguay na Morocco.

Ufaransa ilikuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali baada ya ushindi wake wa mabao 2-0 dhidi ya Morocco na sasa itaivaa Hispania (Julai 14, 2026).

WAKONGWE WAFUNGUKA

Kiungo wa zamani wa timu hiyo, Patrick Vieira, anaamini Ufaransa hii ya kocha Didier Deschamps inaweza kuwa bora zaidi kuwahi kutokea, hasa endapo itatwaa ubingwa Julai 19, 2026.

Dhidi ya Morocco katika mchezo wa robo fainali, Ufaransa ilipata mabao yake mawili ndani ya dakika sita, wafungaji wakiwa ni Kylian Mbappe na Ousmane Dembele.

Kwamba Ufaransa imeingia nusu fainali ikiwa imefunga mabao 16, huku Mbappe akiwa na nane na Dembele akipasia nyavu mara tano.

“Tunazungumzia kizazi chenye wachezaji wengi wazuri na ukiangalia safu ya ushambuliaji, imesheheni kuliko miaka yote. Inafurahisha,” amesema Vieira.

Wakati huo huo, lejendari wa timu ya soka ya Taifa ya Scotland, Pat Nevin, amesema: “Ufaransa ndiyo timu tishio zaidi kwenye ushambuliaji msimu huu.”

Wakati Mbappe na Dembele wakitajwa zaidi, mkongwe wa England, Ian Wright, anasema Ufaransa ina Michael Olise, Bradley Barcola, Desire Doue, Rayan Cherki na Jean-Philippe Mateta.

DESCHAMPS NYUMA YA PAZIA

Deschamps amekuwa kocha wa Ufaransa tangu mwaka 2012 na ameshaweka wazi kuwa atastaafu baada ya kumalizika kwa fainali hizi za Kombe la Dunia.

Katika miaka 14 aliyokaa kwenye benchi la ufundi, Deschamps aliifikisha fainali ya EURO mwaka 2016 lakini walifungwa na Ureno iliyotwaa ubingwa.

Mwaka 2018, kiungo huyo wa zamani aliiongoza Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia, kisha kufika fainali msimu uliofuata (2022), ambapo walifungwa na Argentina.

Katika michuano ya EURO 2024, walifika fainali lakini walishindwa kubeba ‘ndoo’ baada ya kufungwa mabao 2-1 na Hispania.

Safari hii, si tu imefunga mabao 16, pia safu yao ya ulinzi imeruhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili pekee katika mechi zao sita.

ANA KWA ANA NA HISPANIA

Vieira, kiungo wa zamani wa Arsenal, amesema Ufaransa imeimarika zaidi, ikilinganishwa na Hispania ya miaka minne iliyopita.

“Ufaransa ni bora zaidi kwa sasa kuliko ilivyokuwa miaka minne iliyopita. Sioni kama Hispania ya sasa ni nzuri kuliko ile (ya mwaka 2022).

Related articles

Recent articles