29.8 C
New York

Refa huyu alikataliwa na Wafaransa

Published:

BOSTON, Marekani

KATIKA mchezo wa robo fainali uliozikutanisha Ufaransa na Morocco, Facundo Tello raia wa Argentina ndiye aliyekuwa mwamuzi wa kati.

Sasa, weka kando ‘ishu’ ya matokeo ya mechi hiyo iliyochezwa usiku wa Julai 9, 2026, mjini Boston, Marekani.

Tello ana stori yake nyuma ya pazia. Baada tu ya FIFA kumteua, lilizuka zogo, ambapo mashabiki na vyombo vya habari vya Ufaransa wengi vilimpinga. Kwanini?

Refa huyo mwenye umri wa miaka 44, amekuwa akichezesha mechi za Ligi Kuu ya Argentina tangu mwaka 2013.

Pia, kama itakumbukwa, alikuwepo kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizopita zilizofanyika mwaka 2022 nchini Qatar.

Katika michuano hiyo iliyomalizika kwa Argentina kutwaa ubingwa, alichezesha robo fainali ya Morocco na Ureno, ambapo Taifa hilo la Afrika lilishinda bao 1-0.

Hata hivyo, tukio lake kubwa zaidi ni lile la Novemba, 2022. Alitoa kadi nyekundu kwa wachezaji 10 katika mchezo wa Kombe la Ligi nchini Argentina kati ya Racing Club na Boca Juniors.

Mwaka 2024, Tello aliandika historia ya kuwa refa wa tatu kutoka nje ya Ulaya kuchezesha fainali za EURO na alipewa mechi mbili (Uturuki v Georgia na Scotland v Hungary).

Msimu huu wa Kombe la Dunia, mechi ya jana ilikuwa ya tatu baada ya kuchezesha zingine mbili (Canada 1-1 Bosia, Afrika Kusini 1-0 Korea ya Kusini).

Related articles

Recent articles