MANCHESTER, Uingereza
KOCHA mpya wa Manchester City, Enzo Maresca, atatua na watu wapya saba kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.
Maresca ameajiriwa Etihad na kusaini miaka mitatu akichukua nafasi ya Pep Guardiola aliyeondoka mwishoni mwa Juni, 2026.
Ni kama Maresca amerudi nyumbani kwani aliwahi kufanya kazi kwenye timu za vijana za Man City, kabla ya kupandishwa na kuwa msaidizi wa Guardiola.
Miongoni mwa watu saba atakaokuwa nao kwenye benchi ni kipa wa zamani wa Man City, Willy Caballero.
Caballero (46), alistaafu mwaka 2023 akiwa ameitumikia Man City katika michezo 48 kuanzia mwaka 2014 hadi 2017.
Wengine watakaomsaidia Maresca ni Roberto Vitiello, Danny Walker, Denis Silva, Michele De Bernardin, Marcos Alvarez, Javier Molina.


