21.8 C
New York

Kane, Haaland kutunishia misuli robo fainali

Published:

LONDON, Uingereza

NI rasmi sasa timu ya soka ya Taifa ya England itavaana na Norway katika hatua inayofuata ya robo fainali.

Ni michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea katika mataifa matatu ya Marekani, Mexico na Canada.

England ya nahodha Harry Kane ilivuta hatua ya 16 Bora baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji Mexico.

Katika mchezo huo, Kane aliingia kambani mara moja baada ya England Jude Bellingham kufunga mara mbili.

Sasa wana kibarua kigumu cha kupata tiketi ya kucheza nusu fainali kwani watakutana na Norway ya straika Erling Haaland.

Norway ilitinga robo fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa wa zamani, Brazil.

Jahazi la Brazil katika mchezo huo wa hatua ya 16 Bora lilizamishwa na mabao mawili ya nyota huyo wa Manchester City.

Mechi nyingine kali ya hatua ya robo fainali utazikutanisha Morocco na mabingwa wa mwaka 2018, Ufaransa.

Ufaransa waliitoa Paraguay kwa kichapo cha bao 1-0, wakati Morocco waliitandika Canada mabao 3-0.

Related articles

Recent articles