LONDON, Uingereza
KWA fedha nyingi na umaarufu mkubwa walionao, wangeweza kuifanya siku ya ndoa zao kufahamika duniani kote.
Hata hivyo, waliona mambo yasiwe mengi. Wakaamua kufunga ndoa kimyakimya, kisha mashabiki wakajua kupitia picha zilizoachiwa baadaye.
SADIO MANE
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool anayeitumikia Al Nassr ya Saudi Arabia kwa sasa. Mane alimuoa Aisha Tamba kwa ndoa ya siri iliyofungwa Januari, 2024, mjini Keur Massar, Senegal.
CAMERON DIAZ
Bibiye mwenye jina kubwa katika soko la filamu za Marekani (Hollywood). Mwaka 2015, alifunga ndoa ya siri na Benji Madden. Ni baada ya takribani mwaka mmoja wa kuwa naye kwenye mahusiano.
MARTIN ODEGAARD
Nahodha wa Arsenal aliyewahi kupita Real Madrid. Mwishoni wa mwaka 2024, Odegaard alifunga ndoa ya kimyakimya na bibiye Helene Spilling. Watu walikuja kushituka baada ya kiungo huyo kuposti cheti cha ndoa huko mitandaoni.
HARRY MAGUIRE
Beki wa kati wa Manchester United, ambaye alimuoa kimyakimya mpenzi wake wa miaka mingi, Fern Hawkins. Sherehe ya ndoa yao ilihudhuriwa na washikaji zake kadhaa na ndugu wachache wa pande zote mbili.
JAY-Z
Rapa huyo na bibiye Beyonce walifunga ndoa ya kimyakimya Aprili, 2008. Ili kuifanya siri zaidi, sherehe ilifanyika kwenye moja ya nyumba za kifahari za staa huyo wa muziki wa Hip hop.

ILKAY GUNDOGAN
Lejendari wa Manchester City na timu ya soka ya Taifa ya Ujerumani. Alifunga ndoa ya siri na mwanamitindo wa Italia, Sara Arfaoui. Ni baada ya ndoa hiyo, ndipo baadaye wakafanya sherehe kubwa nchini Italia.
IKER CASILLAS
Kipa wa zamani wa Real Madrid, Casillas, alifunga ndoa ya siri na mwandishi wa habari wa Hispania, Sara Carbonero. Ripoti zinaeleza kuwa ni watu watatu pekee walioalikwa kuhudhuria ndoa hiyo iliyofungwa mjini Madrid.
HARRY KANE
Ndoa yake na mpenzi wake wa miaka mingi, Kate Goodland, ilifungwa kwa usiri mkubwa. Ni baada ya mwezi mmoja tangu walipooana, ndipo mshambuliaji huyo wa Bayern Munich alipoachia picha za siku ya ndoa mitandaoni.
DUA LIPA
Bibiye huyo ni supastaa wa muziki wa Pop. Aliamua kufunga ndoa ya kimyakimya na mpenzi wake ambaye ni mwigizaji, Callum Turner. Walivishana pete mwaka 2025 lakini waliifanya siri ndoa hadi picha zilipoibuka mitandaoni.
OXLADE-CHAMBERLAIN
Kiungo wa zamani wa klabu za Arsenal na Liverpool. Alex Oxlade-Chamberlain alifunga ndoa na mpenzi wake, Perrie Edwards. Wawili hao walifunga ndoa ya siri Juni, 2026, na tukio hilo lilifanyika kwa siri nchini Ureno.


