20.6 C
New York

England v Ghana: Refa wa kadi nyingi kusimamia shoo

Published:

NEW YORK, Marekani

UKIWA ni mchezo wa Kundi L, timu ya soka ya Taifa ya England itaivaa Ghana leo Juni 23, 2026 kwenye Uwanja wa Gillette mjini Foxborough, Marekani.

England ‘Three Lions’ imetoka kushinda mabao 4-2 dhidi ya Croatia, wakati Ghana ‘Black Stars’ iliifunga Panama bao 1-0.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limemtangaza Said Martinez kuwa mwamuzi wa kati wa mechi hiyo.

Martinez (34), ni raia wa Honduras na amechezesha mechi moja ya msimu huu wa Kombe la Dunia, akitoa jumla ya kadi za njano tatu na penalti moja (sare ya 1-1 kati ya Qatar dhidi ya Uswis).

Martinez ni refa wa kadi nyingi. Amegawa za njano 691 katika mechi 166 alizochezesha tangu aanze kazi hiyo. Ni wastani wa kadi nne kila mechi.

Kwa upande mwingine, kesho itakuwa mara yake ya kwanza kuchezesha mechi Kati ya England na Ghana.

Pia, Martinez hajawahi kupuliza kipyenga katika mchezo unaoikutanisha timu yoyote ya barani Afrika.

Related articles

Recent articles