MEXICO CITY, Mexico
KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti, amethibitisha kuwa mshambuliaji wake, Neymar, anaweza kuwa fiti kuivaa Scotland katika mchezo wa Jumatano ya wiki ijayo.
Neymar anayekipiga Santos ya Ligi Kuu ya Brazil, alikosekana katika mechi zote mbili za awali msimu huu wa Kombe la Dunia.
Mchezo wa mwisho ni wa jana Juni 19, 2026, ambapo Brazil iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Haiti.
Licha ya ushindi huo, kikosi cha Brazil kilipata pigo baada ya mshambuliaji wake, Raphinha, kupata majeraha yaliyomfanya atolewe katika dakika ya 40.
Endapo ataivaa Scotland, itakuwa mara ya kwanza kwa Neymar kuitumikia Brazil tangu alipocheza Oktoba, 2023, ambapo waliifunga Uruguay mabao 2-0.


