25.1 C
New York

Ibenge aficha silaha za kuibana Yanga

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KOCHA wa Azam FC, Florent Ibenge, amegoma kuanika mbinu za kiufundi atakazozitumia katika mchezo wao dhidi ya Yanga.

Timu hizo zitakutana kesho Juni 21, 2026 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ukiwa ni mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mtanange huo, Ibenge amesema anaiheshimu Yanga kutokana na uimara wake lakini anaamini vijana wake watakuwa bora zaidi ndani ya uwanja.

“Yanga ni timu iliyokamilika kwa kiasi kikubwa na ni ngumu kucheza na timu kama Yanga. Najua kesho Yanga watakuja juu ila Azam FC tutakuwa bora zaidi yao,” amesema.

Kuhusu mbinu atakazotumia mbele ya ‘Timu ya Wananchi’, Ibenge amesema: “Mambo ya kiufundi nitawaambia wachezaji wangu pekee, siwezi kumwambia kila mtu mambo yangu ya kiufundi.”

Katika hatua nyingine, kocha huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), amesisitiza kuwa lengo lao ni kuifunga Yanga na kuingia fainali ya michuano hiyo.

Related articles

Recent articles