25.1 C
New York

Kocha Yanga: Kwa Azam tunataka fainali tu

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MKUU wa benchi la ufundi la Yanga, Abdihamid Moallin, amesema kufika fainali ya FA ni moja ya mipango yao, licha ya ugumu wa wapinzao wao, Azam FC.

Yanga na Azam zitakuwa CCM Kirumba, Mwanza, kesho Juni 21, 2026 kwa mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo msimu wa 2025-26.

Moallin amesema maandalizi ya kuikabili Azam yanaendelea vizuri, ikiwa ni pamoja na wachezaji kuwa fiti kiakili na kimwili, pamoja na kufahamu kile kinachohitajika uwanjani.

“Ni heshima kubwa kucheza nusu fainali ya mashindano kama haya. Tumestahili kufika hapa lakini lengo letu ni kufika fainali. Ili kufanya hivyo, tunapaswa kuwa bora katika wakati huu na kushinda kesho, InshaAllah,” amesema Moallin.

Katika hatua nyingine, kocha huyo amesema wachezaji wa Yanga wana uzoefu mkubwa wa kucheza mechi za aina hiyo, zenye presha kubwa, hivyo anaamini watafanikisha malengo ya kucheza fainali.

Related articles

Recent articles