30 C
New York

Dili zinazotolewa macho usajili wa kiangazi Ulaya

Published:

LONDON, Uingereza

WAKATI huu fainali za Kombe la Dunia zikiendelea, klabu za soka, zikiwamo za Ligi Kuu ya England (EPL) zimeanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao, 2026-27.

Kujipanga huko ni pamoja na kutumia usajili wa dirisha kubwa majira haya ya kiangazi ili kuimarisha vikosi vyao.

ELLIOT ANDERSON (MAN UNITED)

Klabu yake ya Nottingham Forest inataka Pauni milioni 130 ili kumwachia. Manchester United wanaongoza katika mbio za kuinasa saini yake.

Wakati huo huo, Manchester City wanamtolea macho wakiamini atawafaa endapo Rodri atatimkia Real Madrid.

MATEUS FERNADES (ARSENAL)

Kiungo wa mabao matatu na asisti nne msimu uliomalizika wa EPL akiwa na kikosi cha wakongwe wa London, West Ham United.

Arsenal wako mstari kumuwania, licha ya Ma United nao kuhusishwa naye. West Ham wanataka Pauni milioni 80 ili biashara ifanyike.

AYYOUB BOUADDI (LIVERPOOL)

Licha ya Arsenal, Chelsea na PSG, Liverpool imepiga hatua kubwa zaidi katika kuiwania saini ya kiungo huyo wa Lille.
.
Nyota huyo yuko Kombe la Dunia msimu huu akiwa kwenye kiwango bora katika kikosi cha timu yake ya Taifa ya Morocco.

SANDRO TONALI (TOTTENHAM)

Tangu Newcastle ilipomng’oa AC Milan kwa Pauni milioni 60.5, kiungo huyo amecheza mechi 110, alifunga maba 10 na kutoa asisti 10.

Saini yake inawindwa na klabu kadhaa kubwa, ikiwamo Manchester City, lakini ripoti mbalimbali zinaipa nafasi kubwa Tottenham.

ENZO FERNANDEZ (MAN CITY)

Kiungo huyo hataki kubaki Chelsea na alishasema anatamani kuishi katika Jiji la Madrid, wakati huu Real Madrid nayo ikihusishwa naye.

Hata hivyo, huenda Enzo akamfuta Enzo Maresca aliyetua Manchester City kwani ni kocha aliyemfanya kuwa bora wakiwa Stamford Bridge. Blues wanataka Pauni milioni 120

Related articles

Recent articles