LONDON, Uingereza
BAADA ya kunusurika kushuka daraja msimu wa 2025-26 wa Ligi Kuu ya England uliomalizika hivi karibuni, Tottenham imeanza maandalizi ya kuja kivingine.
Chini ya kocha aliyeajiriwa dakika za mwisho na kuiokoa isishuke daraja, Roberto Derbi, Tottenham iko bize kwenye soko la usajili majira haya ya kiangazi.
Tayari imeshawana Andy Robertson na Marcos Senesi kutoka katika klabu za Liverpool na Bournemouth, huku ikiendelea na mazungumzo na Savinho wa Manchester City.
Katika kuimarisha safu ya kiungo, Tottenham imeingia katika mbio za kumsajili staa wa Newcastle United raia wa Italia, Sandro Tonali.
Wakati huo huo, kocha De Zerbi pia ameripotiwa kuipigia hesabu kali saini ya beki wa kati wa Brighton, Jan Paul van Hecke.
Tottenham wamepeleka ofa ya Pauni milioni 30 kwa Brighton lakini klabu hiyo imegoma kupokea na kutaka ipewe mara mbili ya kiasi hicho.


