LAGOS, Nigeria
PACHA wa Kundi la P-Square ambalo limeshavunjika, Peter Okoye, amesema hapendi kuona akifananishwa na kaka yake, Paul.
Wawili hao amekuwa maadui wakubwa kwa siku za hivi karibuni na tangu kuvunjika kwa Kundi, Peter anajiita Mr. P, wakati Paul ni Rudeboy.
Akihojiwa hivi karibuni, Mr. P amesema hataki kufananishwa na Rudeboy wala msanii mwingine yoyote kwenye soko la muziki nchini Nigeria.
“Acheni kunifananisha na kaka yangu au mtu mwingine yeyote. Imetosha kunifananisha. Nataka kuwa mimi na hakuna anayenifikia. Nataka nifanye mambo yangu na kupata pesa,” amesema.
Katika hatua nyingine, Mr. P amesema kitendo cha yeye na kaka yake kuirejesha P-Square miezi michache iliyopita kumeathiri safari yake ya muziki.


