JAKARTA, Indonesia
MWANAUME mmoja nchini Indonesia ameshitakiwa kwa kosa la kumuua mama mzazi wa mke wake, ikielezwa kuwa alimpa mishikaki yenye sumu.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, Purwadi Wahyudi alifikia uamuzi huo Mei 18, 2026 baada ya kuhisi mama mkwe hakuwa akimkubali.
Baada ya kupewa na kula mishikaki yenye sumu, mama mkwe mwenye umri wa miaka 57 akipoteza maisha, kabla ya mawili wake kukutwa ndani na binti yake mwingine.
Inaelezwa zaidi, kwamba Polisi walipochukua mwili wake na kuufanyia vipimo, walibaini kuwa ulikuwa na sumu.
Purwadi mwenye umri wa miaka 40, anashikiliwa na polisi na sheria za Indonesia zinataka ahukumiwe kifungo cha miaka 20 gerezani endapo atakutwa na hatia.


