28.1 C
New York

Hii ndiyo timu yenye wakongwe wengi Kombe la Dunia 2026

Published:

PANAMA CITY, Panama

FAINALI za Kombe la Dunia ziko njiani, zikiwa zimebaki siku tisa pekee kuanza kushuhudia mataifa 48 yakitoana jasho kwa kipindi cha mwezi mmoja wa mashindao hayo.

Moja ya mataifa hayo ni Panama, ambayo timu yake ndiyo iliyojaza wachezaji wenye umri mkubwa zaidi, ikilinganishwa na zingine zitakazoshiriki fainali hizo za Marekani, Mexico na Canada.

Wastani wa umri kwa timu hiyo ya Kundi L ni miaka 30.4. Katika wachezaji 26 walioitwa, 13 wana umri wa miaka 30 au zaidi.

Katika wachezaji 26 hao, ‘mzee’ zaidi ni kiungo  Alberto Quintero, ambaye ana miaka 38 na amecheza mechi 140 akiwa na kikosi cha Panama, akifuatiliwa na nahodha Anibal Godoy, Luis Meija, Eric Davis na Cecilio Waterman, kila mmoja akiwa na miaka 35.

Timu inayoshika nafasi ya pili kwa wachezaji wakongwe ni Colombia, ambayo wastani wa wachezaji 26 walioitwa ni miaka 30.10, wakiongozwa na David Ospina, Camilo Vargas na James Rodriguez.

Aidha, pia zipo Cape Verde, ambayo wastani wa umri kwa wachezaji wake ni miaka 29.61, Brazil (29.18) na Scotland (29.18).

Related articles

Recent articles