28.1 C
New York

Makinda Ecuador kufanya maajabu Kombe la Dunia 2026?

Published:

LONDON, Uingereza

MOJA ya timu za taifa 48 zitakazoshiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu ni Ecuador inayotokea huko Kusini mwa Bara la Amerika. Majirani wa Brazil na Argentina katika eneo hilo.

Usichokijua, Ecuador ndiyo timu yenye wachezaji wenye umri mdogo zaidi msimu huu wa fainali hizo zitakazoanza hivi karibuni (Juni 11, 2026).

Katika wachezaji 26 walioitwa, 12 wana umri chini ya miaka 25 na ni watatu wenye miaka zaidi ya 30. Kwamba wastani wa umri kwa wachezaji wote ni miaka 25.65.

Kikosini, nyota mwenye umri mkubwa zaidi ni kipa Hernan Galindez (miaka 39) na mchezaji mdogo zaidi ni Kendry Paez (miaka 19).

Ivory Coast inashika nafasi ya pili kwa wachezaji wenye wastani wa umri wa miaka 25.8, ikifuatiwa na Morocco (26.3), Tunisia (26.6) na Hispania (miaka 26.7).

Related articles

Recent articles