20.9 C
New York

Virusi hivi vya Ebola vimeshindikana, havina chanzo wala tiba

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MAAMBUKIZI ya virusi vya Ebola yameendelea kuripotiwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kama ilivyo kwa majirani zao, Uganda, huku wataalamu wa afya wakizitahadharisha nchi zingine za Afrika.

Idadi ya vifo kwa upande wa DRC ni zaidi ya 100, huku visa vipya vilivyoripotiwa vikiwa ni zaidi ya 300 katika Jimbo moja la Ituri, ambako ndiko Ebola ilipoanzia.

Wiki chache zilizopita, Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) lilitangaza kuwa Ebola ya safari hii ni dharura ya kiafya inayohitaji msaada wa kimataifa.

Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba Ebola ya safari hii inatofautiana kwa kiasi kikubwa na zingine zilizowahi kuikumba DRC, Uganda na Afrika kwa ujumla.

Ebola hii inasababishwa na virusi aina ya Bundibugyo. Ni aina nyingine ya virusi vya ugonjwa huo ukiacha ‘Zaire’, ‘Sudan’ na ‘Msitu waTai’. Majina hayo yanatokana na eneo ulikoanzia mlipuko.

Tofauti na virusi vingine hivyo, Bundibugyo havina chanjo wala tiba, hivyo kufanya hatari yake kuwa kubwa zaidi.

Katika historia ya Ebola, ni mara tatu pekee imetokea kwa virusi hivyo kuibuka, kwa mujibu wa ripoti ya WHO.

Mara ya kwanza ilikuwa kati ya mwaka 2007 hadi 2008 nchini Uganda, kabla ya kujitokeza tena DRC mwaka 2012. Hata hivyo, havijawahi kuwa na madhara makubwa kama ilivyo sasa.

Tofauti na ilivyo kwa virusi vingine, dalili hujitokeza kwa mgonjwa pale ambapo tayari Bundibugyo vimeshasambaa mwilini, hivyo kuleta ugumu katika kuvidhibiti.

Kama ilivyoelezwa, virusi vya Bundibugyo havina chanzo. Chanzo iliyotumika wakati wa mlipuko wa Ebola miaka michache iliyopita imeshindwa kudhibiti virusi hivyo kwa sasa.

Mbaya zaidi, dalili za mgonjwa wa Ebola itakanayo na virusi hivyo hazina tofauti na magonjwa mengine. Ni homa, uchovu, maumivu ya misuli, kichwa kuuma, kuvuja damu, n.k.

Katika hatua nyingine, hii ni mara ya 17 kwa DRC kukumbwa na mlipuko wa Ebola tangu mwaka 1976. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2025, ambapo ugonjwa huo ilisababisha vifo vya watu 43 katika Jimbo la Kasai.

Related articles

Recent articles