LOS ANGELES, Marekani
KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Marekani, Mauricio Pochettino, ameita kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026 zitakazoanza Juni 11.
Katika kikosi chake, Pochettino raia wa Argentina amewajumuhisha mastaa Christian Pulisic, Weston McKennie na Timothy Weah.
Marekani itakwenda kwenye fainali hizo ikifahamu wazi kwamba imepangwa Kundi lenye timu zisizotabirika za Paraguay, Australia na Uturuki.
Kikosi kilichoitwa na Pochettino, kocha wa zamani wa Espanyol, Tottenham, Chelsea na PSG, ni kama ifuatavyo:
Makipa: Matt Turner (New England Revolution), Fritz (New York City FC) na Chris Brady (Chicago Fire).
Mabeki: Dest (PSV Eindhoven), Chris Richards (Crystal Palace), Robinson (Fulham), Trusty (Celtic), Alex Freeman (Villarreal), McKenzie (Toulouse), na Joe Scally (Borussia M’gladbach).
Viungo: Adams (Bournemouth), Reyna (Borussia M’gladbach), McKennie (Juventus), Aaronson (Leeds United), Miles Robinson (FC Cincinnati), Ream (Charlotte), Berhalter (Vancouver Whitecaps), Cristian Roldan (Seattle Sounders), na Malik Tillman (Bayer Leverkusen)
Washambuliaji: Pepi (PSV Eindhoven), Pulisic (Milan), Arfsten (Columbus Crew), Haji Wright (Coventry), Balogun (Monaco), Timothy Weah (Olympique Marseille) na Sendejas (Club America).


