25.8 C
New York

Olise: Ureno haimtegemei tena Ronaldo

Published:

MUNICH, Ujerumani

WINGA wa Bayern Munich, Michael Olise, amesema kwa sasa timu ya Taifa ya Ureno haimtegemei nahodha wake, Cristiano Ronaldo.

Na badala yake, Olise raia wa Ufaransa amedai kuwa matumaini ya Wareno kuelekea fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu yako kwa kiungo Bruno Fernandes.

Alipoulizwa kwa upande wa England, Olise alimtaja Harry Kane kuwa ndiye mchezaji wao bora kwenye fainali hizo zitakazoanza Juni 11, 2026.

Kwa upande wa Argentina, nyota huyo wa zamani wa Crystal Palace alimtaja Lionel Messi, pia akizungumzia Lamine Hamal kwa timu ya Taifa ya Hispania.

Alipoulizwa kuhusu staa wa Brazil, Olise, ambaye amemaliza msimu wa 2025-26 akiwa na mabao 22 na asisti 31, alisema hajui.

Related articles

Recent articles