TEHRAN, Iran
JESHI la Iran (IRGC) limetangaza kuruhusu meli zaidi ya 30 zilizobeba mafuta kupita katika Mlango-Bahari wa Hormuz usiku wa Mei 14, 2026.
Iran imeimarisha udhibiti wake katika Mlango-Bahari huo tangu iliposhambuliwa na Marekani na Israel miezi takribani mitatu iliyopita (Februari 28, 2026).
Kwa mujibu wa IRGC, katika meli za China ni miongoni mwa zilizoruhusiwa kupita baada ya kukubaliana na utaratibu uliowekwa.
“Ilikubaliwa kuwa baadhi ya meli za China zilizoombewa kibali na nchi hiyo zipite baada ya utaratibu wa Iran kufuatwa,” imeeleza taarifa ya jeshi hilo.
Wakati huo huo, Kamanda wa IRGC ameweka wazi kuwa meli za ‘maadui’ zao zitaendelea kuzuiwa kutumia Mlango-Bahari wa Hormuz.


