14 C
New York

Madarasa 1,360, mabweni 17 na nyumba 33 za walimu kujengwa

Published:

Na Ramadhan Hassan, Gazetini

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepanga kujenga madarasa 1,360 ili kuimarisha utekelezaji wa sera ya elimu ya miaka 10 ya lazima, sambamba na kuongeza miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika shule za msingi na sekondari nchini.

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha mazingira ya elimu na kuongeza upatikanaji wa huduma bora kwa wanafunzi katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, Serikali itajenga mabweni 17 katika shule za sekondari 17 pamoja na nyumba 33 za walimu, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya kazi na makazi kwa walimu, hususan katika maeneo yenye changamoto za miundombinu.

Vilevile, vituo 50 vya walimu vitajengwa katika halmashauri za wilaya kwa lengo la kuongeza motisha kwa walimu na kuimarisha utoaji wa huduma za elimu.

Akizungumza bungeni leo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema, “Serikali imepanga kujenga madarasa 1,360, mabweni 17 na nyumba 33 za walimu ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na kuinua ustawi wa walimu nchini,” amesema Profesa Mkenda.

Profesa Mkenda alitoa kauli hiyo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img