21 C
New York

Infographic| Ukosefu wa elimu ya upangaji bajeti inavyovuruga familia

Published:

KUSUASUA kwa Uchumi ni miongoni mwa sababu ya migogoro kuanzia ngazi ya familia, na wakati mwingine kupelekea uwepo wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.

Inaelezwa migogoro husababishwa na kuyumba kwa uchumi katika ngazi ya familia, wakati mwingine hutokana na kutokuwepo kwa bajeti inayoainisha kipato na matumizi ya familia husika.

Mtaalam wa masuala ya Upangaji wa Bajeti kuanzia ngazi ya familia kutoka Shirika lisilokuwa la Kiserikali la ELIMISHA, Festo Sikagonamo, anasema ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye ngazi ya familia ni muhimu  wanandoa wakapanga bajeti ya familia yao kwa pamoja yenye mlengo wa kijinsia.

Anasema bajeti ya aina hiyo itasaidia familia kuwa yenye furaha kwa sababu mke na mume wakishirikiana kupanga bajeti watafanikiwa kutekeleza majukumu yao kwa pamoja na kuepukana na msongo wa mawazo.

Aidha, anasema kufanya hivyo wanafamilia wataepuka baadhi ya matatizo kama vile ugomvi, kutoaminiana na vipigo ambavyo vimekuwa na madhara makubwa ikiwemo kusababisha vifo.

Baadhi ya migogoro inayotokea kwa wanandoa chanzo kikubwa huwa kuyumba kiuchumi ukiyumba, wanafamilia huishi kwa kuviziana na huishia kwenye ukatili.

Mwanaume hufikiri fedha za matumizi anazoziacha nyumbani huenda mke wake anatumia vibaya, wakati huo mwanamke naye hufikiri mume  anapata kipato kikubwam, lakini hakifiki nyumbani kwa kuwa hawajatengeneza bajeti ya pamoja na hakuna utaratibu wa kupanga kwa siku, wiki na mwezi.

Sikagonamo anafafanua kuwa bajeti inaweza kuwa msaada wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia na kuokoa, maisha ya wanandoa kutokana na msongo wa mawazo, lakini pia kuleta furaha ya maisha.

[googlemaps https://www.google.com/maps?q=MBEYA%2C%20TANZANIA&output=embed&hl=en-US&z=12&w=425&h=350]

Kwa mujibu wa Sikagonamo, miongoni mwa faida ya upangaji bajeti yenye mlengo wa kijinsia ni  kuepusha migogoro ya kugombania mali kwa madai kuwa mume au mke wanaingia kwenye ugomvi kwa sababu wanategemea mali hizo kuendesha maisha  badala ya kufanya shughuli za uzalishaji mali.

Anasema  kwa udadisi waliofanya asilimia 75 ya makundi ya wanawake na vijana hawana elimu ya upangaji bajeti hali inawakwamisha jitihada za kutimiza malengo yao ya kujikwamua kiuchumi. 

Pamoja na hayo kuna tatizo jingine la wanawake kuwa na elimu ya kupanga bajeti, jambo linalosababisha fedha wanayopewa kama mtaji wa biashara kushindwa kuwasaidia na kurudi kuwa tegemezi na mtumwa kwakuwa haruhusiwi kuhoji kipato cha mumewe.

“Uchumi ni miongoni mwa eneo linalochangia ukatili wa kijinsia  kutokana na ukosefu wa elimu ya upangaji bajeti ndani ya familia kwa kiasi kikubwa wanaume ndio huwakatili wake zao hususani wasiokuwana vipato kwa maana ni mama wa nyumbani ili kukabiliana na vitendo hivyo elimu ya upangaji yenye mlengo wa kijinsia inahitajika,” alisema Sikagonamo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, kati ya wanawake 10, saba wamefanyiwa vitendo vya ukatili  wa uchumi na vipigo.

Debora Mwanyanje Mtaalamu wa masuala ya jinsia kutoka Shirika la ELIMISHA, anasema ameshuhudia ndoa nyingi zikivunjika kutokana na ukatili wa kiuchumi, mume kushindwa kuhudumia familia na kumuachia jukumu mwanamke hali inayosababisha msongo wa mawazo na wakati mwingine mtu kulazimika kunywa sumu.

Anasema kina mama wengi hulazimika kuingia kwenye madeni  ili mradi akidhi mahitaji ya familia yake kutokana na waume zao kuwatekeleza wakikwepa majukumu kutokana hali hiyo huchangia msongo wa mawazo.

Regina Sanga Mkazi wa Ilolo anayajishughulisha na kilimo cha mboga, anasema amekuwa msaada mkubwa kwa familia yake kwani licha ya mume wake kufariki dunia miaka kadhaa iliyopita amejitahidi kusomesha watoto na sasa wanajitegemea kwa vipato vyao.

Anasema maisha yake huenda yangekuwa mazuri zaidi endapo angekuwa na elimu ya upangaji wa bajeti kuanzia ngazi ya familia angeweza kuzitumia vyema fedha anazozipata kwenye biashara yake ya kuuza mboga.

Baadhi ya wanaume wamelalamikia wake zao kutokuwa na nidhamu ya fedha wanazoachiwa  kwa ajili ya matumizi ya nyumbani wakidai hupeleka kwenye vikoba na upatu.

Miongoni mwao  anasema kila siku anamuachia Sh 5,000 kwa siku lakini  haandai chakula kinachoendana na hela hiyo na kwamba amebaini mkewe ana matumizi mengine na fedha hizo jambo ambalo ni kinyume na makubaliano na kwamba inachangia ukatili kwa watoto kwani hawapewi chakula kizuri.

Ulimbakisya Mbuto  Mchungaji wa Kanisa la Moraviani Ushirika,   anasema hakuwahi kukaa meza moja pamoja na mkewe kutengeneza bajeti badala yake alimtegemea mkewe kuendesha familia.

Anasema hakuwahi kumpa mkewe hela ya mtaji kwa ajili ya biashara na kwamba laiti angepata elimu ya upangaji bajeti mapema angepiga zaidi hatua za maendeleo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Godfrey Kingamkono, anasema  katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2020 hadi Juni 2021 Halmashauri imetoa mikopo kwa vikundi 70 yenye thamani ya Sh 420.

Anasema vikundi vilivyonufaika ni vya wanawake 28 vimepata shilingi 168 wakiwemo wafanyabiashara na wanaonza kujishughulisha kupitia fedha hizo.

Vilevile vikundi vya vijana 26  kupatiwa shilingi 168 na vikundi vya wenye ulemavu 16 vikipatiwa Sh 84.

Mkoa wa Mbeya kupitia Kamati yake ya Ushauri katika Mwaka wa fedha 2020/2021 kwa Wilaya ya Kyela  imepanga kutumia Sh 252   kwa kuvinufaisha vikundi 26, wanawake vikundi 10, vijana vikundi 10 na watu wenye ulemavu vikundi sita.

Katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, jumla ya vikundi 150 vya wanawake wametengewa fedha kiasi cha Sh milioni 422 na fedha zote tayari zimetolewa kwa vikundi hivyo.

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe jumla ya vikundi vya wanawake 17 vimenufaika na mkopo wenye thamani ya Sh milioni 334.

Kwa mujibu wa Ofisa  ya Maendeleo ya jamii, Stella Kategile anasema mkoa wa Mbeya hadi kufikia Disemba 2020 jumla ya vikundi 94 vya wanawake vimepatiwa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani kiasi cha Sh milioni 571.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img