MANCHESTER, Uingereza
KAMA ukidhani ni utani, basi umepotea. Manchester United imeelekeza nguvu zake zote kwa beki wa kati wa Real Madrid, Antonio Rudiger.
Nyota huyo raia wa Ujerumani ameshacheza mechi 174 tangu alipotua Madrid mwaka 2022 akitokea Chelsea.
Rudiger aliondoka Chelsea akiwa mchezaji huru, hivyo pia kuna uwezekano wa kurudi bure Ligi Kuu ya England, safari hii akielekea Old Trafford.
Ndiyo, mkataba wake na Madrid utakwisha Juni, 2026, na inaripotiwa kuwa ataondoka klabuni hapo.
Wakati Liverpool nayo ikitajwa kumtaka, zipo ripoti kutoka Italia zikidai kuwa Juventus wanamtolea macho.
Juventus wanaamini itakuwa rahisi kumpata kwa kuwa staa huyo ana uhusiano mzuri na kocha wao, Luciano Spalletti, ambaye aliwahi kumnoa wakiwa AS Roma.


