16.3 C
New York

Utafiti: Changamoto wanazopitia makocha wanawake

Published:

LONDON, Uingereza

KWA mujibu wa utafiti wa Taasisi ya Women in Sport kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Leeds Beckett, wanawake waliopo katika taaluma ya ukocha nchini Uingereza wanapitia changamoto kubwa.

Utafiti huo umehusisha mahojiano na makocha 2,000, ambapo asilimia 30 ya wanawake walikiri kupitia unyanyasaji wa kijinsia.

Katika maelezo yao, asilimia 26 walisema walipitia unyanyasaji huo wakiwa hatua za chini za kazi hiyo ya ukocha.

Aidha, asilimia 46 walifichua kuwa wamekuwa wakikumbana na vitendo hivyo, zikiwamo lugha chafu mitandaoni, wakiwa katika ngazi ya juu, kwa maana ya kufanya kazi na klabu kubwa.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Women in Sport, Stephanie Hilborne, anasema jitihada za haraka zinapaswa kufanyika ili kutokomeza utamaduni huo wa makocha wanawake kudharauliwa.

“Lazima ziwepo sera kali, zitakazoambatana na mafunzo, ili kudhibiti tabia za aina hiyo, zinazoondosha usawa katika michezo,” anasema Hilborne.

Aidha, utafiti huo umeenda mbali zaidi na kubaini kuwa wengi hao hawako tayari kuripoti changamoto hizo, licha ya kuwapo kwa taasisi za kuwasaidia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img