15.6 C
New York

Julian Ryerson: Beki, mkali wa ‘asisti’ anayewatoa udenda Man United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

RADA za maskauti wa Manchester United zimemnasa beki wa pembeni wa Borussia Dortmund, Julian Ryerson. Anatakiwa Old Trafford kwa ajili ya msimu ujao.

Ryerson (28), licha ya kwamba ni beki wa kulia, anatumia mguu wa kushoto, hivyo ni kiraka wa maeneo yote mawili ya pembeni.

Achilia mbali takwimu zake nzuri katika kukaba, pia ana ‘asisti’ 14 katika mechi 32 za msimu huu wa mashindano mbalimbali. Kwa Bundesliga pekee, ameshatoa pasi zilizozaa mabao 11.

Sasa, aliyefichua mpango wa Man United kumtaka ni mwandishi wa habari maarufu wa Ujerumani, Ben Jacobs.

Ryerson alianza safari yake ya soka la kulipwa akiwa na Viking FK ya Norway, ambapo alicheza mechi 68, kabla ya kutua Union Berlin ya Bundesliga mwaka 2023.

Akiwa Berlin, alitoa ‘asisti’ tatu katika mechi 109 na ndipo Dortmund ilipomchukua. Ana jumla ya asisti 20 na mabao saba tangu asajiliwe.

Mkataba wake na Dortmund utafikia ukomo Juni, 2028 lakini Man United italazimika kulipa Pauni milioni 26 ili kumsajili mwishoni mwa msimu huu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img