MILAN, Italia
KLABU mbili za Ligi Kuu ya Italia (Serie A), Inter Milan na Juventus, zinapigana vikumbo kuiwania saini ya kipa wa Liverpool, Alisson Becker.
Becker alijiunga na Liverpool ikiwa chini ya kocha Jurgen Klopp wakati wa usajili wa kiangazi, 2018, akitokea AS Roma.
Kwa miaka takribani nane, amecheza mechi zaidi ya 300, pia akiiwezesha Liverpool kutwaa mataji kadhaa, yakiwamo mawili ya Ligi Kuu na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa msimu huu, mlinda mlango huyo wa kimataifa wa Brazil amecheza mara 30 katika michuano mbalimbali.
Inter, kwa upande wao, wanajiandaa na maisha mapya bila Yann Sommer, ambaye huenda akaondoka akiwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.


