13.5 C
New York

Trump aitangazia uadui Hispania

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametishia kusitisha uhusiano wa kibiashara na Hispania, huku Iran ikiwa chanzo cha msuguano huo.

Trump ameeleza nia yake hiyo wakati wa mazungumzo na Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, ambapo aliita Hispania kuwa ni ‘pasua kichwa’.

“Hatutaki uhusiano wowote (wa kibiashara na Hispania),” amesema Trump, ikielezwa kuwa ameshamwagiza Katibu wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, kusitikisha biashara zote na Hispania.

Inaelezwa kuwa Trump amekerwa na kitendo cha Hispania kuonesha kusimama na Iran katika vita inayoendelea, ambapo Marekani na Israel zinashirikiana kuishambulia nchi hiyo.

Utawala wa kijamaa wa Hispania umezuia ndege za kivita za Marekani zilizoko nchini humo kutumikia kuishambulia Iran, Kwa mujibu wa taarifa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img