20.9 C
New York

Clinton akana kuyajua ‘madudu’ ya Epstein

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, amesema hakuwahi kujua maovu ya Jeffrey Epstein hadi pale aliposikia mashitaka yake.

Epstein, mmoja ya matajiri wakubwa nchini Marekani, alifariki akiwa na kashfa za udhalilishaji wa kingono, ikiwamo kuendesha mtandao wa biashara ya kuwauza wasichana na wanawake.

Lakini, kwa wiki za hivi karibuni yameibuka mafaili yanayofichua maovu yake. Zipo picha na video zinazomuonesha Epstein akiwa na watu maarufu, akiwamo Clinton.

Clinton, licha ya kukiri kuwa rafiki wa Epstein, amesema hakujua chochote na aliachana muda mrefu na Epstein, kabla ya kuanza kusikia maovu yake yakifichuliwa.

Kwa mujibu wake, alianza kuwa na ukaribu na Epstein mwaka 2002 lakini urafiki wao huo ulidumu kwa miezi michache tu.

“Sikuona chochote kibaya nilipokuwa karibu naye. Sikuona chochote kilichoashiria anajihusisha na usafirishaji wa wanawake,” amesema.

Related articles

Recent articles