20.9 C
New York

City yamtolea macho kiungo Bundesliga

Published:

MUNICH, Ujerumani

MANCHESTER City imeendelea kuipambania saini ya kiungo wa Borussia Dortmund, Felix Nmecha, ambaye anatajwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 60.

Kwa mujibu wa mtangazaji wa kituo cha runinga cha Sky nchini Ujerumani, Patrick Berger, kocha wa Man City, Pep Guardiola, yuko ‘siriazi’ na usajili huo.

Berger amenyetisha kuwa Dortmund nao wanapambana kumshawishi nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 kusaini mkataba mpya.

Tayari Mkurugenzi wa Michezo wa Dorrmund, Sebastian Kehl, ameanza mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji huyo, kwa mujibu wa Berger.

Wakati huo huo, zipo taarifa zinazodai kuwa klabu zingine za England zinazomtolea macho ni pamoja na Manchester United.

Related articles

Recent articles