6.4 C
New York

Mourinho: Madrid? Siwezi kurudi

Published:

LISBON, Ureno

KOCHA wa Benfica, Jose Mourinho, ameziita kuwa ni uzushi taarifa zinazomuhusisha na kibarua cha kuinoa Real Madrid.

Waandishi wa habari walimuuliza Mourinho juu ya uwezekano wa kukataa endapo Rais wa Madrid, Florentino Perez, atamuomba kurudi Santiago Bernabeu.

Katika jibu lake, ‘Special One’ alisema ndiyo, kwamba anaweza kukataa endapo Perez atampa ofa ya kufanya tena kazi klabuni hapo.

“Huwa sipendi kuzungumzia mambo ambayo hayapo. Jambo lililopo ni kwamba nina mkataba na Benfica.

“Ni mkataba maalumu kwa kuwa ulisainiwa wakati wa mchakato wa Uchaguzi wa rais katika klabu hii,” amesema.

Mreno huyo aliajiriwa na Perez mwaka 2010 baada ya kufanya vizuri akiwa na Inter Milan, ambapo alitwaa mataji matatu kwa mpigo.

Akiwa Madrid, kocha huyo wa zamani wa Chelsea alishindwa kuipa taji la Ligi ya Mabingwa lakini aliweza kutwaa mataji mengine matatu (La Liga, Copa del Rey na Spanish Super Cup), kabla ya kuondoka mwaka 2013.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img