6.4 C
New York

Arsenal kuchomoa kinda Madrid

Published:

LONDON, Uingereza

ARSENAL inaongoza katika mbio za kuiwania saini ya kinda wa Real Madrid,  Victor Valdepenas, kwa mujibu wa Gazeti la AS la Hispania.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya wakubwa (dhidi ya Alaves) mwanzoni mwa msimu huu.

Kwa upande wao, Arsenal wanavutiwa naye kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.

Mbali ya kucheza vizuri beki wa kushoto, pia Valdepenas anaweza kutumika kama mlinzi wa kati kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza mipira ya juu.

Licha ya Washika Bunduki kutajwa kuongoza, mbio za kuiwania saini yake zinazihusisha pia klabu za AC Milan, Bayer Leverkusen na Borussia Dortmund.

Katika eneo la beki wa kushoto, tayari kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, anao Riccardo Calafiori, Piero Hincapie na Myles Lewis-Skelly.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img