9 C
New York

United yagoma kumwachia Rashford

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KLABU ya Barcelona sasa ina kazi ngumu kumbakiza Marcus Rashford baada ya Manchester United kusema straika huyo hauzwi.

Barcelona ilimchukua kwa mkopo wa msimu mmoja na sasa mshambuliaji huyo ni tishio Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).

Rashford amefunga mabao tisa na kutoa ‘asisti’ tisa katika mechi 29 za La Liga na Ligi ya Mabingwa alizocheza.

Ni kutokana na kiwango chake hicho, Barcelona wanajaribu kuishawishi Man United ikubali kuwauzia Muingereza huyo.

Kwa upande wao, Man United wamegoma kuzungumzia biashara hiyo, na badala yake wanataka Rashford arudi Old Trafford.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img