CATALUNYA, Hispania
KLABU ya Barcelona imetangaza usajili wa beki wake wa zamani, Joao Cancelo, na tayari amekabidhiwa jezi namba 2.
Barcelona imemchukua nyota huyo kwa mkopo kutoka Al Hilal ya Saudi Arabia, ikiwa ni miezi 18 tu tangu alipoondoka Camp Nou.
Kwa mara ya kwanza, Cancelo, alitua Barcelona kwa mkopo akitokea Manchester City na ni baada ya kukorofishana na Pep Guardiola.
Akiwa chini ya kocha Xavi, nyota huyo alikuwa na kiwango bora, ambapo alifunga mabao manne na kutoa ‘asisti’ tano.
Hata hivyo, Barcelona walikataa kumsajili moja kwa moja, licha ya kwamba walitakiwa kuipa Manchester City kiasi cha euro milioni 25 tu.


