MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid, Xabi Alonso, amewataka mabosi wa klabu hiyo kuharakisha usajili wa beki wa Tottenham, Cristian Romero.
Romero ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi pale Tottenham, Pauni 200,000 kwa wiki, na mkataba wake wa sasa utakwisha mwaka 2029.
Madrid inahitaji beki wa kati, hasa ikizingatiwa kuwa zipo taarifa za David Alaba kutohitajika pindi atakapomaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Pia, taarifa zinaeleza kuwa Madrid haina mpango wa kumpa mkataba mpya mlinzi mwingine wa kati raia wa Ujerumani, Antonio Rudiger.
Kwa sasa, Alonso haoni kama kinda Dean Huijsen ameiva kuaminiwa, wakati huo pia kiwango cha Raul Asencio kikiwa hakijaimarika vya kutosha.
Licha ya ubora wa Eder Militao, changamo kubwa ya beki hiyo wa kimataifa wa Brazil ni majeraha ya mara kwa mara, kama ilivyo kwa Alaba na Rudiger.


