10.6 C
New York

Arsenal, City zamgombea beki Newcastle

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Arsenal imejitosa kuiwania saini ya beki wa Newcastle United, Tino Livramento, ambaye pia anaitoa udenda Manchester City.

Livramento aliibuliwa na ‘academy’ ya Chelsea na mwaka 2021 alitwaa tuzo ya Kinda Bora wa Mwaka klabuni hapo.

Kutokana na kukosa namba katika kikosi cha timu ya wakubwa, Livramento aliondoka Stamford Bridge mwaka huo na kujiunga na Southampton.

Mlinzi huyo wa pembeni aliondoka Southampton mwaka 2023 baada ya kuvutia Newcastle iliyotumia Pauni milioni 40 kumsajili.

Haa hivyo, Arsenal wao hawatarajiwi kumsajili Januari hii na badala yake watasubiri majira ya kiangazi mwishoni mwa msimu huu.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, anatazamiwa kwenda kuziba pengo la Ben White anayetarajiwa kuondoka baada ya kukosa namba kikosi cha kwanza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img