15 C
New York

Kocha Barcelona: Hatukustahili ushindi

Published:

CATALUNYA, Hispania

KOCHA wa Barcelona, Hans Flick, amedai kuwa timu yake ilionesha kiwango kibovu katika mchezo dhidi ya Espanyol, hivyo haikistahili kupata ushindi wa mabao 2-0.

Ulikuwa ni mchezo wa La Liga uliochezwa jana Januari 3, 2026, ambapo Barcelona walikuwa ugenini dhidi ya wapinzani wao hao wakubwa.

Kwa matokeo hayo, Barcelona waliendeleza ushindi woa wa mechi tisa mfululizo za Ligi Kuu hiyo ya Hispania.

Akizungumza baada ya dakika 90, Flick raia wa Ujerumani amesema hakufurahishwa na kiwango cha timu yake.

“Kuna mambo ya kufanyia kazi, ingawa nimefurahia ushindi wa pointi tatu. Tunapaswa kujua kuwa Espanyol walicheza vizuri. Hatukustahili kupata ushindi,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img