6.4 C
New York

Miji inayoongoza kwa mabilionea wengi duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

NEW YORK ndiyo Mji unaoongoza kwa kuwa na mabilionea wengi duniani, kwa mujibu wa Jarida maarufu la Forbes.

Mji huo wa Marekani unatajwa na Forbes kuwa na mabilionea 109, ukifuatiwa na Hong Kong wa China wenye mabilionea 74.

Moscow nchini Urusi ni Mji wa tatu kwenye orodha hii, ukiwa na mabilionea 73, wakati Mumbai wa India unashika nafasi ya nne kwa mabilionea 69.

Mji Mkuu wa China, Beijing, uko nafasi ya tano, ambapo Forbes wanautaja kuwa na mabilionea 63.
Katika orodha ya Forbes, Mji Mkuu wa Uingereza, London, unafuata katika nafasi ya sita kwa mabilionea 62, ukifuatiwa na Shanghai wa China wenye mabilionea 54.

Miji mingine na idadi ya mabilionea wake ni kama ifuatavyo; Singapore (52), San Francisco (50), New Delhi (43) na Shenzhen (37).

Pia, ipo miji ya Los Angeles (35), Taipei (34), Hangzhou na Seoul (31), Paris (28), Tokyo (27), Bangkok na Milan (26), na Dallas (24).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img