15 C
New York

Arsenal, Chelsea kukutana robo fainali Ligi ya Mabingwa?

Published:

LONDON, Uingereza

NI Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa soka la wanawake, ambapo huenda hatua ya robo fainali ikawashuhudia mabingwa watetezi, Arsenal, wakavaana na Chelsea.

Hata hivyo, majirani hao wa London watakutana endapo Arsenal wataitoa Leuven ya Ubelgiji katika mechi mbili za ‘play-off’.

Chelsea wao walitinga hatua ya robo fainali baada ya kumaliza ndani ya ‘Top Four’ katika kundi walilokuwa na Barcelona, Lyon na Bayern Munich.

Wakati huo huo, Manchester United wataivaa Atletico Madrid katika mechi nyingine ya play-off na mshindi wa jumla ataikabili Bayern Munich katika hatua ya robo fainali.

Kwa upande mwingine, mabingwa mara nane wa Ligi ya Mabingwa, Lyon, watatoana jasho na mshindi wa play-off kati ya Wolfsburg na Juventus katika hatua hiyo ya robo fainali.

Aidha, Barcelona, ambao walifika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, wao wameshaingia robo fainali na sasa wanasubiri mshindi kati ya Paris FC na Real Madrid.

Mechi za play-off zinatarajiwa kuanza kuchezwa Februari 11, mwakani, huku zile za robo fainali zikisubiriwa Machi 24, mwakani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img