15 C
New York

Mbappe bado bao moja tu

Published:

MADRID, Hispania

STAA wa Real Madrid, Kylian Mbappe, amebakiza bao moja kufikia rekodi ya mkongwe wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo.

Katika mchezo wa jana Desemba 17, 2025 dhidi ya Talavera, Mbappe mwenye umri wa miaka 26 alifunga mara mbili na Madrid kupata ushindi wa 3-2.

Mchezo huo dhidi ya timu ya Ligi Daraja la Tatu nchini Hispania ulikuwa wa Copa del Rey na ushindi walioupata Madrid umewapeleka hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

Mbappe amefikisha mabao 58 na kubakiza moja kumfikia Ronaldo ambaye ndiye mchezaji wa Madrid mwenye rekodi ya kufunga mara nyingi ndani ya mwaka mmoja.

Ronaldo anayekipiga Al Nassr ya Saudi Arabia kwa sasa, alifunga mabao 59 akiwa na Madrid mwaka 2013.
Akiwa amebakiza bao moja, huenda Mbappe akaifikia na hata kuivunja rekodi hiyo endapo atafunga katika mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Sevilla.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img