12.6 C
New York

Kocha Newcastle mbioni kutimuliwa

Published:

LONDON, Uingereza

IKIWA ni miaka minne tangu alipoajiriwa Novemba 2021, kocha Eddie Howe ameingia kwenye hatari ya kufungashiwa virago katika klabu ya Newcastle United.

Newcastle imekuwa na mwenendo usioridhisha katika mechi zake za Ligi Kuu ya England (EPL), ikiwamo kufungwa bao 1-0 na Sunderland hivi karibuni.

Licha ya kwamba ni kipigo pekee katika mechi tano za EPL zilizopita, Howe anakabiliwa na presha kubwa kwa kuwa timu hiyo iko nje ya ‘Top 10’ kwenye msimamo wa Ligi Kuu hiyo.

Kutokana na mwenendo huo, Howe mwenye umri wa miaka 48 amekuwa akikosolewa vikali na mashabiki wa Newcastle huko mitandaoni.

Hata hivyo, zipo taarifa zinazodai kuwa mabosi wa Newcastle hawashawishiki na ukosowaji unaofanywa na mashabiki juu ya kocha huyo.

Ni kwa maana hiyo, mabosi watampa muda, ikizingatiwa kwamba bado Newcastle inafanya vizuri Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Ligi (Carabao Cup).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img