CATALUNYA, Hispania
MWANAMFALME wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, ametenga kitita cha euro bilioni 10 ili kuinunua klabu ya Barcelona.
Aliyefichua mpango huo ni mwandishi wa habari za michezo wa Gazeti la El Chiringuito la Hispania, Francois Gallardo.
Barcelona ni moja ya klabu zenye thamani kubwa duniani na Kwa sasa inatajwa kufikia Pauni bilioni 4.1.
Salman, ambaye wakati fulani alihusishwa na mpango wa kuinunua Manchester United, ana utajiri wa Pauni bilioni 18.7.
Kwa upande mwingine, familia yake ya kifalme inatajwa kuwa na utajiri unaofikia Pauni trilioni moja.
Barcelona inapitia kipindi kigumu kwa upande wa masuala ya uchumi, ikikumbukwa kuwa ilitumia Pauni milioni 23 pekee katika dirisha la usajili lililopita.


