12.6 C
New York

Kane aiokoa Bayern kwa ‘bao la jioni’

Published:

MUNICH, Ujerumani

BAO la dakika ya 87 la Harry Kane limeiwezesha Bayern Munich kuambulia sare ya mabao 2-2 ikiwa nyumbani dhidi ya Mainz katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).

Lennart Karl alitanguliza Bayern kwa bao la dakika ya 29, kabla ya Kacper Potulski kuisawazishia Mainz (dk. 45).

Katika dakika ya 67, Mainz walipata bao la pili kupitia Jae-sung Lee aliyefunga kwa kichwa akiunganisha pasi ya Stefan Bell.

Zikiwa zimebaki dakika tatu mchezo huo kumalizika, Kane aliangushwa kwenye boksi na Potulski na kupata penalti aliyopiga na kuiwezesha Bayern kuokoa pointi moja.

Kwa sasa, nahodha huyo wa timu ya taifa ya England ‘Three Lions’ ndiye kinara wa mabao msimu huu wa Bundesliga akiwa ameingia kambani mara 18.

Aidha, mpachikaji mabao huyo amefikisha mabao 80 tangu alipotua Bundesliga akitokea Ligi Kuu ya England (EPL) alikokuwa akiitumikia Tottenham. Bayern watashuka tena dimbani Jumapili ijayo kwa kwa mchezo wa ugenini wa Bundesliga dhidi ya Heidenheim.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img