12.6 C
New York

Mashabiki wa Messi wang’oa viti India

Published:

NEW DELHI, India

MASHABIKI wa Lionel Messi wamekasirishwa na hatimaye kuamua kung’oa viti baada ya kunyimwa fursa ya kumuona kwa muda mrefu staa huyo wa soka. Messi aliwasili India na kufika katika Uwanja wa Salt Lake mjini Kolkata, ambapo maelfu ya mashabiki walijaa kumtazama.

Hata hivyo, licha ya kutozwa kiingilio cha Pauni 100, mashabiki walishuhudia Messi akitumia dakika 20 pekee, kisha akaondoka zake.

Mbaya zaidi, kile kilichowatibua mashabiki ni kwamba hawakupewa muda wa kutosha wa ‘kujiachia’ naye, na badala yake nafasi hiyo waliipata viongozi na mastaa.

Ni kutokana na hasira hizo, mashabiki walianza kuzomea, kabla ya kung’oa viti na kutupa vitu uwanjani. Mmoja ya mashabiki alisema:

“Ni viongozi na waigizaji tu waliokuwa wanamzunguka Messi … Kwanini walituita sasa. Tulinunua tiketi kwa Rupia 12,000 lakini hata kuuona uso wa Messi ilikuwa shida.”

Katika ziara yake nchini India, Messi aliweza pia kuzindua sanamu yake yenye urefu wa futi 70 mjini Kolkata.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img