Na mwandishi wetu, Gazetini
HIYO ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wataalamu wa afya wanaojihusisha na masuala ya homoni nchini Ujerumani.
Katika utafiti wao, wamebaini kuwa midoli ya plastiki, licha ya kupendwa na watoto, inaathiri ukuaji na hata afya yao ya uzazi.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, midoli ya plastiki ina kemikali maarufu ya Endocrine disruptors (EDCs), ambayo hata kiasi kidogo tu cha harufu yake huathiri utendaji wa homoni.
Aidha, mbali ya midoli ya plastiki, utafiti huo umeeleza kuwa kemikali hizo za EDCs hupatikana pia katika vipodozi vinavyotumiwa zaidi na wanawake.
“Hizi kemikali zinaweza pia kupatikana katika mazingira yetu ya kila siku, ikiwamo katika vipodozi, vyombo vya plastiki, rangi na midoli ya bei rahisi ya watoto,” anasema Dk. Josef Kohrle.
Mwisho, katika utafiti wao huo, wataalamu wa afya wanawashauri wazazi kuwaepusha watoto wao na matumizi ya midoli ya plastiki.
Wanaonya, kwamba huenda wengi wakadhani midoli ya zamani haina kemikali hizo, jambo ambalo si sahihi hata kidogo.
“Kemikali aina ya EDC zina uwezo mkubwa wa kuendelea kuwa hai hata katika vitu vya plastiki vilivyoharibika,” anasema Dk. Kohrle.


