12.6 C
New York

Ekitike aweka rekodi bao la mapema EPL

Published:

MERSEYSIDE, England

KATIKA ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Brighton, straika wa Liverpool, Hugo Ekitike, alifunga yote na kuandika historia mpya msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Ekitike raia wa Ufaransa alifunga bao la sekunde ya 46, likiwa ni la mapema zaidi tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu hiyo. Kwa kufanya hivyo, Ekitike anakuwa mchezaji wa kwanza kuifungia Liverpool bao la mapema tangu Naby Keita alipofanya hivyo mwaka 2019.

Keita raia wa Guinea ya Ikweta, alifunga bao la sekunde ya 15 katika mchezo wao dhidi ya Huddersfield Town na Liverpool kushinda mabao 5-0. Wakati huu Keita akiwa Ferencvaros ya Hungary, Ekitike ameendelea kuonesha kiwango bora katika mechi za hivi karibuni akiitumikia Liverpool.

Nyota huyo wa zamani wa Eintracht Frankfurt ameshafikisha mabao tisa, yakiwamo matatu katika mechi mbili za hivi karibuni kwenye Ligi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img