12.7 C
New York

Mastaa wanaosubiriwa EPL dirisha dogo Januari

Published:

LONDON, Uingereza

USAJILI wa dirisha dogo wa Januari, mwakani, uko njiani kwa klabu za soka barani Ulaya, zikiwamo zile za Ligi Kuu ya England (EPL).

Manchester United inaendelea kuhusishwa na mpango wa kuongeza mshambuliaji, wakati huo Liverpool wakiripotiwa kusaka mbadala wa Mohamed Salah anayetaka kuondoka Anfield.

Ivan Toney (West Ham)

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Watford anayekipiga Al Ahli ya Saudi Arabia, ameingia kwenye rada za West Ham, pia Tottenham nayo ikihusishwa naye kwa siku za hivi karibuni.

West Ham wanahitaji straika kwa kuwa Callum Wilson haonekani kumudu jukumu hilo, huku Niclas Fullkrug akihusishwa na mpango wa kuondoka.

Rodrigo Mendoza (Arsenal)

Arsenal wanahusishwa na kinda huyo, ingawa wanakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa vigogo wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A), Juventus.

Kiungo huyo wa Elche anatajwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 17.5, kiasi ambacho Arsenal waliwahi kukitumia kumsajili Sambi Lokonga.

Mike Maignan (Chelsea)

Chelsea wanahitaji mlinda mlango wa kusaidiana na Robert Sanchez baada ya Joao Pedro kuonekana kushindwa kuwa kwenye kiwango bora cha ushindani.

Blues wangeweza kumsajili Maignan wakati wa usajili wa kiangazi, mwaka huu, lakini waligoma kuipa AC Milan kiasi kidogo tu cha Pauni milioni 20.

Conor Gallagher (Man United)

Manchester United iko kwenye harakati za kumsajili kiungo huyo wa Atletico Madrid. Taarifa zinaeleza kuwa wanamtaka Gallagher kwa mkopo.

Ni usajili wa kiungo wa kati, ingawa kocha Ruben Amorim amekuwa pia akihusishwa na Elliot Anderson, Adam Wharton na Carlos Baleba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img