9.8 C
New York

Kombe la Dunia 2026; Kundi L

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KUMEKUCHA! Droo ya hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia ilichezeshwa nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza, fainali hizo zitashirikisha mataifa 48, huku mechi 104 zikitarajiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya Marekani, Mexico na Canada.

Tukijikumbushe; timu 42 zilishakata tiketi na sasa zinasubiriwa zingine sita zitakazopatikana kupitia mechi za ‘play-off’ zitakazochezwa Machi, mwakani.

Sasa, makala haya yanaliangazia Kundi L na kuchambua timu zilizopo kuelekea michuano hiyo itakayoanza Juni 11, mwakani.

Ni katika Kundi lenye England, Croatia, Ghana na Panama. Thomas Tuchel aliajiriwa na kupewa sharti moja tu; kuipa England ubingwa wa Kombe la Dunia.

‘Three Lions’ walikata tiketi wakiwa hawajaruhusu bao. Hata hivyo, bado safi ya ushambuliaji imekuwa ikimtegemea zaidi nahodha wake, Harry Kane.

Katika Kundi hili, pia ipo Croatia ya kocha mzawa na mwenye uzoefu mkubwa, Zlatko Dalic. Walifuzu wakiwa wamedondosha pointi mbili pekee.

Ghana, maarufu pia kwa jina la ‘Black Stars’, haitoshiriki fainali za AFCON za mwaka huu, lakini itakwenda Kombe la Dunia hapo mwakani.

Ikiwa na mastaa Antoine Semenyo, Mohammed Kudus, Inaki Williams, Abdul Fatawu na Jordan Ayew, ilikata tiketi ikiwa imefungwa mechi mbili kati ya 10.

Panama, kwa upande wao, hii ni mara ya pili kushiriki Kombe la Dunia. Safari hii, walifuzu bila kufungwa katika raundi ya mwisho kwa Ukanda wa Concacaf.

Historia inawakumbusha mashabiki wa Panama kwamba waliruhusu mabao sita walipokutana na England katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 kule Urusi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img