11.6 C
New York

Kombe la Dunia 2026; Kundi J

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KUMEKUCHA! Droo ya hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia ilichezeshwa nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza, fainali hizo zitashirikisha mataifa 48, huku mechi 104 zikitarajiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya Marekani, Mexico na Canada.

Tukijikumbushe; timu 42 zilishakata tiketi na sasa zinasubiriwa zingine sita zitakazopatikana kupitia mechi za ‘play-off’ zitakazochezwa Machi, mwakani. Sasa, makala haya yanaliangazia Kundi J na kuchambua timu zilizopo kuelekea michuano hiyo itakayoanza Juni 11, mwakani.

Katika Kundi hili, zipo Argentina, Algeria, Austria na Jordan. Baada ya miaka 28 ya ukame wa mataji, Argentina wametwaa Kombe la Dunia na Copa America ndani ya miaka minne tu ya hivi karibuni.

Argentina wamefuzu wakiwa kileleni mwa Kundi katika mechi za Ukanda wa wao wa Conmebol. Je, Lionel Messi atakayekuwa na umri wa miaka 39 hapo mwakani bado atakuwa na nguvu ya kuibeba timu hiyo?
Algeria ya kocha Vladimir Petkovic inakwenda kwa mara ya tano kwenye fainali za Kombe la Dunia. Ni mabingwa wa AFCON mwaka 2019.

Austria iko chini ya kocha mzawa aliyewahi pia kuinoa kwa muda mfupi Manchester United, Ralf Rangnick. Walifuzu Kombe la Dunia kwa kuifunga Bosnia katika mchezo wa mwisho.

Kama ilivyo kwa Austria, Iran nayo ipo Kundi hili, pia ikiwa haipewi nafasi kubwa ya kufanya maajabu kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia.

Kikosi cha Iran kinanolewa na kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco, Jamal Sellami, ambaye ni muumini wa mfumo wa 3-4-3.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img